Posts

Showing posts from April, 2023

46 - Miguuni Pake Yesu

46 - Miguuni Pake Yesu "Sitting At The Feet Of Jesus" 1. Miguuni pake Yesu, Maneno yake tamu; Pahali palipo heri, Niwepo kila siku. Miguuni pake Yesu, Nakumbuka upendo Nahisani vyake kwangu, Vimenivuta moyo. 2. Miguuni pake Yesu, Hapa pahali bora Pakuweka dhambi zangu, Pahali pa pumziko. Miguuni pake Yesu, Hapa nafanya sala, Kwake napewa uwezo, Faraja na nehema. 3. Unibariki Mwokozi, Ni miguuni pako, Unitazame kwa pendo, Nione uso wako. Nipe Bwana nia yake, Ili ionekane Nimekaa na Mwokozi, Aliye haki yangu.  (Amina)

47 - Ni Heri Kifungo

47 - Ni Heri Kifungo "Blest Be The Tie" 1. Ni heri kifungo Kinachotufunga Mioyo yetu kwa upendo Pendo la Kikristo 2. M-bele ya Baba Tunatoa sala; Hofu, nia, masumbufu Yetu ni moja. 3. Tunavishiriki Matata na shida, Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka. 4. Tunapoachana Moyoni twalia; Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.   (Amina)

48 - Ninakupenda Zaidi

48 - Ninakupenda Zaidi "I Know I Love Thee Better, Lord" 1. Ninakupenda zaidi, Ya vyote vingine; Kwani umenipa raha, Na amani, Bwana. Nusu haijatangazwa (tangazwa) Ya upendo wako; Nusu haijatangazwa (tangazwa) Damu hutakasa (takasa). 2. Nakujua u karibu Kuliko dunia; Kukukumbuka ni tamu Kupita kuimba. 3. Kweli wanifurahisha, Na nitafurahi; Pasipo upendo wako Naona huzuni. 4. Itakuwaje Mwokozi, Kukaa na wewe, Ikiwa ulimwenguni, Tuna furaha hii? (Amina)

49 - Ninaye Rafiki

49 - Ninaye Rafiki "I 've found A Friend" 1. Ninaye rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo lake Nimefungwa milele. Aukaza moyo wangu, Uache ugeuzi, Ninakaa ndani yake, Yeye Kwangu, milele. 2. Ninaye Rafiki ndiye, Aliyenifilia; Alimwaga damu yake, Kwa watu wote pia. Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele, Pia vyote ni amana, Ndimi wake milele. 3. Ninaye Rafiki naye, Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu `tachukuliwa; Nikitazama mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele. 4. Ninaye Rafiki naye, Yuna na moyo mwema; Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga, Na mpenzi wa mbele? Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.  (Amina)

50 - Mungu Nawe Nanyi Daima

50 - Mungu Nawe Nanyi Daima      "God Be With You!" 1. Mungu nawe nanyi daima; hata twonane ya pili, Awachunge kwa fadhili, Mungu nawe nanyi daima. Hata twonane juu, hata twonane tena kwake; Hata twonane juu, Mungu nawe nanyi daima. 2. Mungu nawe nanyi daima; awafunike mabawa, Awalishe, awakuze; Mungu nawe nanyi daima. 3. Mungu nawe nanyi daima; kila wakati wa shida Awalinde hifadhini; Mungu nawe nanyi daima. 4. Mungu nawe nanyi daima; awabariki na pendo Ambalo halina mwisho; Mungu nawe nanyi daima.  (Amina)

51 - Kuwa Na Yesu Mwokozi

51 - Kuwa Na Yesu Mwokozi "Blessed Assurance" 1. Yesu Mwokozi, kwa hakika, Hunipa furaha na amani; Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake. Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu. Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu. 2. Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana; Aniletea malaika, Wananilinda, niiokoke. 3. Hali na mali anitwaa, Katika Yesu nabarikiwa; Nikimgoja kwa subira, Wema wake unanitosha.  (Amina)

52 - Nipe Biblia

 52 - Nipe Biblia "Give Me The Bible" 1. Nipe Biblia nyota ya furaha, wapate nuru wasafirio; Hakuna la kuzuia amani, Kwani Yesu alituokoa. Nipe Biblia neno takatifu, Nuru yako itaniongoza, Sheria na ahadi na upendo, Hata mwisho vitaendelea. 2. Nipe Biblia nihuzunikapo ikinijaza moyoni dhambi ; Nipe neno zuri la Bwana Yesu, Nimwone Yesu Mwokozi wangu. 3. Nipe Biblia nipate kuona, hatari zilizo duniani; Nuru ya neno lake Bwana Yesu, Itaangaza njia ya kweli. 4. Nipe Biblia taaa ya maisha; Mfariji tunapofiliwa; Unionyeshe taa ya mbinguni, Nione utukufu wa Bwana (Amina)

53 - Napenda Kuhubiri

  53 - Napenda Kuhubiri "I Love To Tell The Story" 1. Napenda kuhubiri habari ya Yesu, Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu. Kuhubiri napenda kwa hali na mali: Mwanyewe nimeonja, najua ni kweli. Napenda kuhubiri kisa cha Bwana Yesu. Ya Bwana wa fahari na pendo zake kuu. 2. Napenda kuhubirimambo ya ajabu Na tukiya fikiri yapita dhahabu. Kuhubiri napenda ya yaliyonifaa: Nami sasa napenda hayo kwa kuimba. 3. Napenda kuhubiri, hunifurahisha Tamu yake habari haiwezi kwisha. Napenda kuhubiri wa gizani nao; Hawana muhubiri wa kweleza chuo. 4. Kuhubiri napenda hata wajuao; Kusikia hupenda kama wenzi wao. Nakao kwenye fahari nikiimba wimbo. Nitaimba habari za Mwokozi huyo. (Amina)

54 - Nataka Nimjue Yesu

54 - Nataka Nimjue Yesu "More About Jesus" 1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili. Zaidi, zaidi,nimfahamu Yesu Nijue upendo wake, wokovu wake kamili. 2. Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu. 3. Nataka tena zaidi, daima kupambanua Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza. 4. Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu. Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake.   (Amina)

55 - Twapanda Mapema

55 - Twapanda Mapema "Sowing In The Morning" 1. Twapanda mapema na mchana kutwa Mbegu za fadhili hata jioni Twangojea sasa siku za kuvuna; Tutashangilia wenye mavuno. Wenye mavuno wenye mavuno, Tutasha ngilia wenye mavuno; Wenye mavuno wenye mavuno, Tutasha ngilia wenye mavuno. 2. Twapanda mwangani  na kwenye kivuli Tusishindwe na baridi na pepo Punde itaisha kazi yetu hapa Tutashangilia wenye mavuno. 3. Twapana kwa Bwana mbegu kila siku. Tujapoona taabu nahuzuni;  Tuishapo shinda atatupokea: Tutashangilia wenye mavuno. (Amina)

56 - Waponnye Watu

56 - Waponnye Watu "Rescue The Perishing" 1. Walio kifoni, nenda waponye. Uwatoe walio shimoni; Wanaoanguka uwainue; Habari njema uwajulishe. Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko huwangojea 2. Wajapokawia anangojea Awasubiri waje tobani; Mwokozi hawezi kuwadharau, Huwasame he tangu zamani: 3. Na ndani ya moyo wa wanadamu Huwapo shida, tena huzuni; Lakini kwa Yesu kuna rehema Kuwaponya na kuwaokoa. 4. Walio kifoni, nenda waponye Kazi ni  yetu, zawadi iko; Nguvu kuhubiri Bwana hutoa Kwa subira tuwavute sasa. (Amina)

57 - Usikatae Kazi

57 - Usikatae Kazi "Ask Not To Be Excused" 1. Usiikatae kazi yake Bwana; Ukae tayari kuifanya kazi; Uende po pote Mungu akwitapo, Nawe utaona furaha kazini Njoo, We! Usikatae; Njoo, We! Uifanye kazi; Usiikatae kazi yake Bwana, Ili hatimaye usikatazwe juu. 2. Usiikatae kazi yake Bwana; Kwa nini kawia? Fanya kazi leo. Mavuno meuoe, Wachache wavuni, Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana. 3. Usiikatae kazi yake Bwana; Kukataa pendo Kwako ni hatari. Saa ya rehema, Yesu akiomba, Ziungame dhambi, Zifutwe mbinguni.   (Amina)

58 - Zitakuwa Nyota Tajini?

58 - Zitakuwa Nyota Tajini?   "I Am Thinking Today" 1. Leo nina fikiria nchi nzuri Ninayotaka kuiona; Nisimamapo karibu na Mwokozi, Tajini zitakuwa nyota? Sijui tajini mwangu kama nyota  Zitang`aa kila wakati! Nitakapoamka katika majumba Zitakuwa nyota Tajini? 2. Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, Nitavuta roho za watu, Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu. 3. Nitakuwa na furaha nikimwona, Kuweka miguuni pake Watu walio vutwa kwa ajili ya Kazi yangu na Roho yake.   (Amina)

59 - Fanyeni Kazi Zenu

59 - Fanyeni Kazi Zenu "Work For The Night Is Coming" 1. Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali; Kesheni saa zenu vumilieni; Kwa Yesu tumikeni na hiyo injili. Sana wahubirini watu wa mbali. 2. Fanyeni kazi zenu, giza yasongea; Nawengi wenzi wenu wamo gizani. Msipoteze moja dakika ni hizi: Bwana atarejea mwisho wa kazi. 3. Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa; Wote walio kwenu apenda Mungu: Na sisi tumjuaye tuwafundishe Ili Yesu ajaye tumfurahishe.  (Amina)

60 - Nitakwenda Utakaponituma

60 - Nitakwenda Utakaponituma "It May Not Be On The Mountain Height" 1. Pengine sio milimani Utakaponiita Pengine sio baharini Wala palipo vita; Lakini unaponiita, Na njia siijui. Bwana, nitajibu, ni tayari Kwanda uniagizapo. Ukiwa pamoja nami, Bwana, Mlimani, baharini, Niende utakaponiita; Na fuata uendako. 2. Pengine leo kuna neno, Neno tamu la pendo, Ambalo Yesu anataka Ninene kwa upole; Ukiwa pamoja nami, Bwana, Nitamtafuta leo Yele aliyepotea mbali: Nitasema upendavyo 3. Pahali pako bila shaka Pa kuvuna shambnani, Kazi niwezayo kufanya Kwa Yesu Mkombozi; Hivi nikikutegemea, Kwa kuwa wanipenda, Mapenzi yako nitafanya, Na niwe upendavyo. (Amina)

61 - Bwana Nami

61 - Bwana Nami "I Have A Friend So Precious" 1. Nimemwona rafiki wa thamani kubwa, Ananipenda kwa ‘pole, kwa pendo amini: Kuishi kute ngwa naye, la, huki siwezi, Tunakaa pamoja: Bwana nami. 2. Pengine nimechoka, mimi mdhaifu, Ndipo ninamtegemea, alivyoalika; Huniongoza njiani, pahali pa nuru, Twatembea pamoja: Bwana nami. 3. Namweleza huzuni, na fura ha yangu, Vile ninavyosumbua, vinavyopendeza; Huniagiza kutenda, yanayonipasa, Twazungumza pamoja: Bwana nami. 4. Ajua natamani, kuwavuta watu, Hivyo ananipeleka, kutangaza Neno; Nitangaze pendo lak, kwa niniakafa; Twahubiri pamoja: Bwana nami.   (Amina)

62 - Napenda Kitabu Chake

 62 - Napenda Kitabu Chake "I Love The Sacred Book" 1. Napenda kitabu chake, kilichotoka mbinguni, Barua kwangu ya Bwana Ujumbe wake wa`pendo. 2. Humo ndani ya kitabu Sura ya Yesu naona; Karatasi zimekuwa, Wayo zake za Mwongozi. 3. Mapenzi yake Mwumbaji, Kubwe la asali tamu; Natamani kuuonja, Ule mkate wa uzima. 4. Mapenzi Yake Mwumbaji, Yanafunuliwa humo; Hazina kuu ya hekima, Utajiri wa ajabu. 5. Mwangaza wa ulimwengu Angaza humo moyoni! Uwe mwandamizi pote, Taa ya hatua zangu. (Amina)

63 - Niuonapo Msalaba

63 - Niuonapo Msalaba "When I survey The Wonderous Cross" 1. Niuonapo msalaba, Kristo aliponifilia; Kwangu pato ni hasara. Kiburi nakichukia. 2. Na nisijivune, Bwana, Ila kwa sadaka yako; Upuzi sitaki tena, Zi chini ya damu yako. 3. Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu, Ndako pweke hamu hiyo. Pendo zako zimetimu. 4. Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha; Pendo zako zaniwia, Nafsi, mali, na maisha. (Amina)

64 - Piga Panda Ya Injili

64 - Piga Panda Ya Injili "Watchman, Blow THe Gospel Trumpet' 1. Piga panda ya Injili, onyesha watu wote; Ili anayesikia atubu, aokoke. Piga panda ya Injili, upige kwa nguvu; Mungu amekuagiza mateka wawe huru. 2. Upige vilimani, kwa kila tambarare; Pande zote, miji yote isikie Injili. 3. Uipige mipakani, barabarani pia; Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba. 4. Uipige! Watu wengi wataka wawe huru; Waambie kwamba Yesu asema "Njoni kwangu."  (Amina)

65 - Twendeni Askari

65 - Twendeni Askari "Onward Christian Soldiers" 1. Twendeni askari, Watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, Tumwandame juu; Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini. Twendeni Askari, Watu wa Mungu;  Yesu yuko mbele, Tumwandame juu; 2. Jeshi la shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia;  Kelele za shangwe zivume pote; Ndugu, inueni zenu sauti. 3. Kweli kundi dogo, watu wa Mungu, La mababa yetu ni letu fungu; Hatutengwi nao, moja imani; Tumaini moja, na moja dini. 4. Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa yake Mfalme; Juu hata chini sana zivume.   (Amina)

66 - Roho Yangu Amka Sasa

66 - Roho Yangu Amka Sasa "Awake My Soul" 1. Roho yangu amka sasa, mara jitahidi; Shindano ni lake Bwana, zawadi ni taji. 2. Sauti ni yake Mungu inayokuita; Ndiyo aliyekirimu taji ya uzima. 3. Mashaidi ndio wengi wanao kuona; Ya nyuma usifikiri bali mwendo kaza. 4. Bwana umetuanzisha katika shindano; Kwa vile tunaposhinda ushindi ni wako. (Amina)

067 - Kesha Roho Yangu

067 - Kesha Roho Yangu "My Soul Be On Thy Guard" 1. Kesha roho yangu, adui maelfu Hujaribu kuangusha, kuvuta dhambini. 2. Ukeshe, uombe, ili ushindwe; Fanya vita kila siku, omba msaada. 3. Kushinda ni bado: ulinde silaha; Usiache kupigana hata una taji.   (Amina)

68 - Tusimame Imara Mwambani

  68 - Tusimame Imara Mwambani "Firmly Stand For God" 1. Umtetee Mungu duniani ijapo pepo kali za vuma; Mwambani pekee pana nguvu Dhambi ikimea. Tusimame imara katika mwamba, Mwamba wa Kristo pekee; Ndipo salamini tutasimama Kule kitini pa enzi. 2. Itetee haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani; Mwambani pekee utashinda wingi wa upotovu. 3. Itetee kweli, itadumu, ijapo kawia itashinda; Mwambani pekee pana raha yaishapo tufani. (Amina)

69 - Cha Kutumaini Sina

69 - Cha Kutumaini Sina "My Hope Is Built" 1. Cha kutumaini sina ila damu yake Bwana,  Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha. Kwake Yesu nasimama, Ndiye mwamba: ni salama; Ndiye mwamba: ni salama; 2. Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga nguvuzake ndizo nanga. 3. Damu yake na sadaka nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha. 4. Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani; Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.   ( Amina)

70 - Wapenzi Wa Bwana

70 - Wapenzi Wa Bwana "Come We That Love The Lord" 1. Wapenzi wa Bwana ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha, Imbeni nyimbo za raha; Za ibada yenu, za ibada yenu. Twenenda Zayuni, mji mzuri Zayuni! Twenenda juu Zayuni, Ni maskani ya Mungu. 2. Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio, Watoto wa Mungu ndio, Waimbao chini, waimbao chini, 3. Twaona rohoni baraka za Mungu, Tusijafika mbinguni, Tusijafika mbinguni, Kwenye utukufu, kwenye utukufu. 4. Tutakapomwona masumbuko basi, Huwa maji ya uzima, Huwa maji ya uzima,Anasa halisi, anasa halisi. ( Amina)